• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maafisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wasikitishwa na Marekani kujitoa kwenye Baraza la haki za binadamu la Umoja huo

    (GMT+08:00) 2018-06-20 17:16:27

    Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bw. Zeid Al-Hussein jana ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Marekani kujitoa kwenye Baraza la haki za binadamu la Umoja huo.

    Bw. Zeid Al-Hussein amesema, kutokana na hali ya haki za binadamu ya hivi sasa duniani, Marekani inapaswa kusonga mbele, na si kurudi nyuma.

    Mwenyekiti wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Bw. Vojislav Suc ametoa taarifa akisisitiza umuhimu wa Baraza hilo, vilevile amesema Baraza hilo limetoa mchango mkubwa katika miaka 12 iliyopita baada ya kuundwa.

    Licha ya hayo, ujumbe wa kudumu wa Umoja wa Ulaya mjini Geneva nao umetoa taarifa ukisema, Umoja wa Ulaya unakisikitika na uamuzi wa Marekani, na utaendelea kuunga mkono kazi ya bodi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako