• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya kibiashara ya Marekani yataka bunge kusimamia zaidi sera za kibiashara za rais Trump

    (GMT+08:00) 2018-06-20 17:28:24

    Kundi la mashirikisho 60 ya biashara nchini Marekani limelitaka bunge kusimamia kwa makini zaidi matumizi ya kodi na hatua nyingine za sera za kibiashara zinazotumiwa na rais Domald Trump wa nchi hiyo.

    Katika barua yao kwa Kamati ya Fedha ya Bunge iliyotolewa jana, mashirika hayo yameeleza wasiwasi wao na mwelekeo wa sera za biashara za Marekani, hususan utayari wa utawala wa sasa kutumia kodi kama msingi mkuu wa sera katika migogoro ya kibiashara inayoongezeka kati ya mashirika hayo na wadau wao.

    Mashirikisho hayo yamesema kodi kubwa kupita kiasi na uwezekano wa vita ya kibiashara na wenzi wao, vinaleta hali ya wasiwasi ambayo itawakumba Wamarekani wote na sekta zote za biashara nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako