• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wakimbizi milioni 5 wa Afghanistan warejea makwao katika miaka 16

    (GMT+08:00) 2018-06-20 17:29:18

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, zaidi ya wakimbizi milioni 5.2 wa Afghanistan wamerejea nchini kwao katika miaka 16 iliyopita.

    Taarifa hiyo imetolewa leo, ambapo dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi. Shirika hilo limesema, ukosefu wa upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya, nyumba, na ardhi bado ni changamoto kubwa kwa wakimbizi wanaorejea nchini Afghanistan kujenga upya maisha yao.

    Waziri wa Masuala ya Wakimbizi Sayed Hussain Alemi Balkhi jana alisema, karibu raia milioni 6 wa Afghanistan bado wanaishi kama wakimbizi katika nchi za Pakistan na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako