• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China na kiongozi wa Korea Kaskazini wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-06-20 18:51:46

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un.

    Rais Xi amesema, hii ni mara ya tatu kwa Bw. Kim Jong-un kukutana naye ndani ya siku 100, na wameweka historia mpya ya mawasiliano ya viongozi wa nchi hizo mbili. Ameleza imani yake kuwa uhusiano kati ya China na Korea Kaskazini utanufaisha zaidi nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Bw. Kim Jong-un amesema ziara hiyo ni fursa za kuzidisha urafiki kati yake na rais Xi na kukuza uhusiano kati ya Korea Kaskazini na China. Amesema Korea Kaskazini itashirikiana na China kuonesha umuhimu kwa ajili ya kulinda amani na utulivu wa kikanda na wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako