• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yateua gavana mpya wa benki kuu

    (GMT+08:00) 2018-06-20 19:21:11
    Ethiopia imemteua gavana mpya wa benki kuu nchini humo ikiwa ni hatua ya kuleta mageuzi ya kichumui

    Gavana mpya huyo bwanaYinager Dessie awali alihudumu kwenye tume ya mipango ya kitaifa ya mipango inayohusika na sera za kiuchumi.

    Hatua hii inafuatia mabadiliko makubwa ya kisera yalianza kutekelezwa miezi miwili iliopita.

    Aidha serikali imetangaza mapema mwezi huu kuwa itauza hisa zake kwenye sekta ya mawasilian, shirika la ndege na nyinginezo.

    Uuzaji huo wa hisa za mashirika ya serikali ni sehemu ya msururu wa hatua alizotangaza waziri mkuu mpya Abiy Ahmed ili kumaliza mgogoro wa kisiasa na kiuchumi wa muda mrefu.

    Abiy ameliambia bunge kwamba serikali itauza kati ya asilimia 30 na 40 za Ethio Telecom.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako