• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • JKU yakamilisha maandalizi ya awali

    (GMT+08:00) 2018-06-21 08:36:06
    Klabu ya JKU ya Zanzibar tayari imekamilisha mazoezi ya awali na kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mashindano ya kombe la Kagame yanayoandaliwa na baraza la vyama vya michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

    Katibu wa klabu hiyo Sadu Ujudi Maalim amesema, timu yake iko tayari kwa mapambano kwenye michuano hiyo na wamejipanga kuleta ushindani na kujifunza kwa timu zingine.

    Wakati huohuo, timu za APR ya Rwanda na Singida United ya Tanzania zimeteuliwa kushiriki kwenye michuano hiyo badala ya St. George ya Ethiopia na Yanga ya Tanzania.

    Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza Juni 28 hadi July 12 jijini Dar es Salaam Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako