• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wa Kenya kufaidika na mkopo wa EU

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:22:48

    Wakulima wadogo wadogo nchini Kenya wanatarajiwa kufaidika na mfuko wa shilingi bilioni 11 zilizotolewwa na Umoja wa Ulaya kusaidia kuimarisha teknolojia za kilimo.

    Mpango uliozinduliwa hivi karibuni wa AgriFi Kenya na Umoja wa Ulaya unalenga kuongeza ushindani miongoni mwa wakulima wadogo na pia kuwafungulia nafasi zaidi za kuuza mazao yae kwenye masoko ya nje.

    Fedha hizo ni pamoja na euro milioni 45 kutoka umoja wa Ulaya na euro milioni 50 kutoka benki ya uwekezaji ya Ulaya na wakulima wataweza kuzipata kupitia kwa benki za kibiashara kwa mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako