• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaweka "Siku ya mavuno ya wakulima" ili kuhimiza ustawi vijijini

  (GMT+08:00) 2018-06-21 20:11:21

  Waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu leo hapa Beijing ametangaza kuwa, kuanzia mwaka huu China itaweka siku ya nusu ya majira ya mpukutiko (Autumnal Equinox) kwa kalenda ya kilimo ya China kuwa "Sikukuu ya mavuno ya wakulima ya China", ambayo ni siku ya kwanza inayowekwa na serikali ya China kwa ajili ya wakulima.

  Bw. Han Changfu amesema kwenye mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, "Siku ya mavuno ya wakulima ya China" imewekwa katika mchakato wa China wa kutekeleza Mikakati ya kustawisha vijiji", anasema:"Hatua hii inaweza kuwahamasisha wakulima kujishughulisha na mambo ya kustawisha vijiji pia itaweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa mikakati ya ustawi vijijini. Mbali na hayo itaweza kukidhi mahitaji ya wakulima kuishi maisha mazuri. Msingi wa ustawi vijijini ni maisha yenye utajiri wa mali na hali."

  Bw. Han Changfu amedokeza kuwa siku ya mavuno ya wakulima ya China kwa mwaka huu itakuwa tarehe 23 Septemba, ambapo shughuli mbalimbali zenye umaalumu zitafanyika ili kufanya jamii na wakulima wote wafurahie mavuno ya kilimo.

  Pia ameeleza kuwa China ina desturi ya kusherehekea mavuno mazuri ya kilimo na kutarajia amani na usalama wa nchi na watu, hali ambayo imeipa China uzoefu wa kuweka sikukuu hiyo ya wakulima. Wakati huo huo, mambo ya kilimo ya China yamepata maendeleo kwa kasi, hali ambayo imeweka msingi mzuri wa kuwekwa kwa sikukuu hiyo. Bw. Han Changfu anasema:"Tangu sera ya mageuzi ilipoanza kutekelezwa, mapato ya wakulima yamekuwa yakiongezeka, huku mchakato wa mambo ya kisasa ya kilimo ukiharakishwa, na maendeleo ya uchumi yasiyo na uchafuzi wa mazingira, mageuzi ya vijiji, na marekebisho ya miundo pia yamepata maendeleo kwa udhahiri, aidha Jamii ya vijijini inadumisha utulivu kwa muda mrefu, hayo yote yameweka msingi imara kwa ajili ya siku ya mavuno ya wakulima ya China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako