• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Argentina yachungulia mlango wa kutokea, Mbappe aisogeza Ufaransa 16 Bora,

  (GMT+08:00) 2018-06-22 08:37:50

  Timu ya Argentina haikuamini macho yao kwa kipigo cha usiku wa kuamkia leo cha jumla ya magoli 3-0 toka kwa Croatia katika michuano ya kundi D ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Urusi.

  Magoli matatu ya kipindi cha pili yametosha kabisa kupunguza kasi ya Argentina kusonga mbele katika michuano hiyo. Argentina inatakiwa sasa kupata ushindi mnono dhidi ya Nigeria ili kujiweka katika nafasi nzuri kwani hadi sasa anapointi 1 tu.

  Mechi iliyopigwa uwanja wa Ekaterinburg baina ya Ufaransa na Peru, imeshuhudia Kylian Mbappe wa Ufaransa akiiweka timu yake kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua ya 16 bora baada ya kufunga goli dakika ya 34 dhidi ya Peru kwenye mchezo wa kundi C.

  Nayo Denmark imelazimishwa sare ya goli 1-1 na Australia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako