• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Challenge ya Wanawake sasa kufanyika Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-06-22 08:38:53

    Mashindano ya kuwania kombe la Challenge kwa upande wa wanawake kwa nchi za Afrika Mashariki na kati sasa yatafanyika kuanzia Julai 19 hadi 29 nchini Rwanda.

    Awali mashindano hayo yanayoandaliwa na baraza la soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yalitarajiwa kuanza Mei 12 hadi 22 mwaka huu lakini yalisogezwa mbele kutokana na sababu zisizozuilika.

    Katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika.

    Nchi ambazo zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Rwanda, mabingwa watetezi Tanzania, Kenya, Uganda, Djibouti, Zanzibar na Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako