• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yazipiga faini Mexico na Serbia.

    (GMT+08:00) 2018-06-22 08:40:41
    Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limezipiga faini Mexico na Serbia kwa makosa ya kumtusi kipa Manuel Neuer na kuweka bango lenye ujumbe wa siasa uwanjani.

    Mexico imepigwa faini baada ya mashabiki wake kuonyesha kitendo cha ubaguzi kwa kipa Neuer wa Ujerumani zilipokutana Juni 17, timu ya Mexico ilishinda mechi hiyo ya kundi F kwa bao 1-0.

    Serbia imeadhibiwa kwa kuweka bango lenye ujumbe wa kisiasa ilipokuwa ikimenyana na Costa Rica Juni 17, Serbia ilishinda mchuano huo wa Kundi E kwa bao 1-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako