• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa sera ya kufungua mlango

  (GMT+08:00) 2018-06-22 16:45:49

  Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alipokutana na wakuu wa mashirika makubwa ya kimataifa walioko China kuhudhuria mkutano wa kilele wa kamati ya watendaji wakuu duniani, amesema China imetekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa miaka 40, na inaamini kuwa sera hiyo ni njia muhimu ya kuhimiza maendeleo ya taifa.

  Jana Rais Xi Jinping alikutana na watendaji wakuu wa mashirika makubwa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Australia na nchini nyingine kuzungumzia masuala mbalimbali, ikiwemo pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, uvumbuzi, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, na usimamizi wa mambo ya kimataifa. Anasema,

  "China imetekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa miaka 40. Mashirika yenu ni mashuhuda wa utekelezaji wa sera hiyo."

  Rais Xi amesema katika miaka 40 iliyopita, mabadiliko makubwa yametokea nchini China, uchumi umeendelea kwa kasi na mfululizo, huku watu zaidi ya milioni 700 wakiondokana na umaskini kwa mujibu wa vigezo vya Umoja wa Mataifa. Anasema,

  "Katika hali mpya, China haitasimamisha sera ya kufungua mlango. Tuna malengo makubwa zaidi na tutaendelea na sera hiyo kwa ufanisi zaidi."

  Rais Xi amesema tangu mwaka jana, uchumi wa dunia umekuwa na mwelekeo mzuri, lakini bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali, haswa vitendo vya kujilinda kibiashara. Anasema,

  "Katika hali mpya, tunapaswa kukabiliana na changamoto kwa ushirikiano na mshikamano, ili kupata mafanikio ya pamoja. Tunatetea kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kuona kuwa mambo ya kimataifa yanapaswa kushughulikiwa na nchi zote kwa pamoja, na mafanikio ya maendeleo pia yanapaswa kuzinufaisha nchi zote."

  Rais Xi amesema tangu miaka mitano iliyopita lilipotolewa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", pendekezo hilo limewanufaisha watu wa nchi husika, na China inayahamasisha mashirika ya kimataifa kujiunga na pendekezo hilo, ili kupata mafanikio ya pamoja.

  Aidha rais Xi amesisitiza kuwa uwekezaji wa nchi za nje umetoa mchango muhimu katika maendeleo ya uchumi na utekelezaji wa sera ya mageuzi nchini China. Mafanikio ya China katika miaka 40 iliyopita yamepatikana kutokana na sera ya kufungua mlango, na China itafungua mlango zaidi katika siku zijazo. Anasema,

  "Kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi wa Asia la Boao uliofanyika April mwaka huu, nilitangaza hatua mpya za China za kufungua mlango zaidi, na hivi sasa zinatekelezwa."

  Wajumbe wa mashirika wamesema wakati mashirika ya kimataifa yanapotoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya China, pia yananufaika kwa muda mrefu, pendekezo la China la Ukanda mmoja na Njia Moja linalingana na mahitaji ya zama, na kuleta ustawi kwa nchi husika, na mashirika hayo yanapenda kujiunga na pendekezo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako