• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Umoja wa Mataia wapongeza mafanikio ya China katika kupambana na UKIMWI

    (GMT+08:00) 2018-06-22 16:58:50

    Maofisa wa Umoja wa Mataifa wamesifu mafanikio yaliyopatikana nchini China katika kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.

    Akizungumza wakati wa ziara yake nchini China, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibe amesema kutokana na uongozi imara, uvumbuzi na wabia wake, China imepata maendeleo makubwa katika kupambana na ugonjwa huo. Pia mkurugenzi huo amepongeza juhudi za China katika miaka ya karibuni kwenye kuboresha upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na tiba.

    Naye mwakilishi mkazi wa Shirika hilo nchini China Amakobe Sande amesema, juhudi za China katika kupambana na UKIMWI ni za kipekee kutokana na idadi kubwa ya watu, na kwamba kilichomvutia zaidi ni kuwa, China inapoahidi, inatekeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako