• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mbaazi yaanza kupanda Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:23:33

    Wizara ya Kilimo ya Tanzania imesema hali iliyosababisha kuporomoka kwa bei ya mbaazi nchini humo ilikuwa ni kutokana na ongezeko la uzalishaji wa zao hilo katika nchi za India, China, Brazil, Myanmar, Canada, Msumbiji, Sudan na Tanzania.

    Naibu Waziri Dk Mary Mwanjelwa amesema bei ya zao hilo iliporomoka kutoka wastani wa bei ya Sh 2,750 kwa kilo mwaka 2014/15 hadi Sh 700 kwa msimu wa mwaka 2015/16 na kufikia wastani wa Sh 300 kwa msimu wa mwaka 2016/17 katika mikoa mbalimbali nchini.

    Kauli hiyo inakuja wakati ambapo wakulima wa mbaazi mikoa ya Mtwara na Lindi wameshuhudia kuporomoka kwa bei katika msimu wa mwaka huu pamoja na kwamba walihamasika kulima kwa wingi.

    Dk Mwanjelwa amesema pamoja na ongezeko hilo la uzalishaji mwezi Agosti 2017 nchi ya India ambayo ndio wanunuzi wakuu wa mbaazi zao ilizuia uingizaji wa mbaazi kutoka nje ya nchi hiyo kwa kuwa walikuwa na uzalishaji mkubwa wa kukidhi mahitaji yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako