• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maduka yatakiwa kupima sukari waliyonayo madukani

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:24:21

    Mkurugenzi wa Afya ya Umma Dkt Kepha Ombacho ameyataka maduka ya jumla kupima sukari waliyo nayo ili kuthibitisha ikiwa inakidhi viwango vya ubora.

    Ombacho ameonya kuwa sukari itakayopatikana haijatimiza viwango vya ubora itaondolewa madukani na kupigwa marufuku.

    Amesema tayari wamebaini kuwa sukari hatari kwa afya tayari inauzwa madukani.

    Msako umeshika kasi baada ya kubainika kuwa Wakenya wamekuwa wakitumia sukari iliyochanganywa na madini ya shaba na mekyuri ambayo ni hatari kwa afya na yanaweza kusababisha maradhi ya kansa yanapoingia mwilini.

    Katika Kaunti ya Meru, Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) jana ilinasa magunia 3,000 ya sukari inayoshukiwa ni ya magendo.

    Kamishna wa Kaunti ya Meru Wilfred Nyagwanga alisema sukari hiyo ambayo iliingizwa nchini kutoka Brazil, ilipatikana ikipakiwa kwenye mifuko ya kuonyesha kuwa ilitoka Zambia.

    Watu 13 ambao walifumaniwa wakipakia sukari hiyo katika mifuko mipya walikamatwa pamoja na mmiliki wa duka hilo.

    Mjini Kitale, polisi walifanikiwa kunasa sukari zaidi ya magunia 550 ambayo ilikuwa imefichwa na mfanyibiashara mmoja inayoshukiwa ni ya kutoka nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako