• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yasema haitafuti tozo kwenye daraja la Kigamboni

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:24:51

    Serikali ya Tanzania imesema kuwa haitafuta tozo inayotozwa katika daraja la Kigamboni kwa kuwa fedha hizo zinatumika kulipa sehemu ya deni la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

    Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Antony Mavunde ameisema kwa sasa utaratibu unaandaliwa ili wavukaji wawe na hiari ya kulipa kwa siku, wiki au mwezi kulingana na uwezo wa mtu.

    Bw Mavunde alikuwa akizungumza bungeni baada ya kuombwa kueleza tangu kujengwa kwa daraja hilo Serikali imekusanya kiasi gani cha fedha kinachotokana na malipo kwa wanaovuka pamoja na vyombo vya moto.

    Bunge pia limeitaka serikali kuweka utaratibu wa kutumia kadi maalum (smart card) kulipia kwa mwezi malipo kwa wanaovuka daraja hilo. Mavunde amesema Serikali kupitia NSSF ndio wanaosimamia daraja hilo.

    Hadi kufikia Machi mwaka huu, NSSF ilikusanya Sh 19.73bilioni tangu daraja hilo lilipoanza kutumika Mei 2016. Amesema kwa sasa NSSF ipo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi wa kuweka mfumo utakaotumia kadi maalum 'Smart Card' kwa malipo ya wanaovuka darajani hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako