• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tatu wa vijana wa China na Afrika wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-06-23 19:02:19

    Mkutano wa tatu wa vijana kutoka China na Afrika umefanyika hivi karibuni hapa Beijing, China, na kuhudhuriwa na wajumbe 70 ambao wamebadilishana maoni kuhusu mawasiliano ya utamaduni.

    Ofisa wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika Zhou Yuxiao amesema, China inakubali na kuheshimu utamaduni wa Afrika, na kutilia maanani mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika katika mambo ya utamaduni.

    Mjumbe kutoka Tanzania Hellen Urio amesema mawasiliano ya tamaduni tofauti yanawawezesha watu kutathmini na kurithi vizuri zaidi utamaduni wao. Ameongeza kuwa, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini Beijing utaleta nafasi nyingi zaidi kwa ajili ya mawasiliano ya utamaduni kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako