• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Tanzania aishukuru serikali ya kwa fursa za elimu inayotoa kwa watanzania

    (GMT+08:00) 2018-06-25 09:57:44

    Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki ameishukuru serikali ya China kwa udhamini inaotoa kwa wanafunzi wa Tanzania hapa China, na fursa nyingine za elimu na mafunzo inayotoa kwa Tanzania. Balozi Kairuki ametoa shukurani hizo wakati watanzania 342 waliokuwa wanasoma katika vyuo mbalimbali hapa China, ikiwa ni wale wanaosoma kwa udhamini na wanaojilipia, wanahitimu masomo yao.

    Balozi Kairuki pia ametumia nafasi hii kufahamisha juhudi zinazofanywa na ubalozi wa China kutafuta fursa zaidi za elimu kwa ajili ya watanzania wanaotaka kupata mafunzo ya ufundi kazi. Tayari vyuo kadhaa vimeahidi kutoa nafasi za udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako