• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Ufaransa

    (GMT+08:00) 2018-06-25 19:21:54

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Ufaransa Bw. Edouard Philippe.

    Rais Xi Jinping amesema, China inapenda kutimiza pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuunganisha mikakati ya maendeleo ya Ufaransa na Umoja wa Ulaya, kwa kushikilia kanuni ya kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaisha kwa pamoja, na kwamba pande mbalimbali zinapaswa kushikilia msimamo wa pande nyingi, haki na usawa, na kulinda kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa.

    Bw. Phillippe amesema, Ufaransa unapenda kuongeza mawasiliano ya uchumi, biashara na utamaduni kati ya nchi hizo mbili, kuhimiza ushirikiano katika matumizi ya kiraia ya nishati ya nyuklia na safari za anga ya juu. Ufaransa inapenda kushirikiana na China kuhimiza amani na utulivu wa dunia, na kuimarisha uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na China.

    Hii ni ziara ya kwanza kwa waziri mkuu huyo nchini China baada ya kushika madaraka tarehe 22 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako