• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miradi ya wajibu kwa jamii ya China yaleta tabasamu Kenya

    (GMT+08:00) 2018-06-25 19:42:38

    Kampuni ya China inayotekeleza mradi wa reli ya kisasa nchini Kenya CRBC imesema itaendelea kusaidia jamii zinazoishi karibu na reli hiyo ambayo sasa iko kwenye awamu ya pili kuendelea Naivasha.

    Akizungumza kwenye hafla ya kutoa ripoti ya miradi yake ya wajibu kwa jamii, mwenyekiti wa kampuni hiyo, bwana Lu Shan amesema bali na kujenga shule na kuchimba visima kwa jamii, pia wamejihusisha na njia bora za ujenzi ambazo haziathiri mazingira au wanyama pori.

    Wanafunzi wa shule ya msingi ya AIC Kitet kaunti ya Narok nchini Kenya wakikariri shairi la kupongeza kampuni ya CRBC kwa kuwajengea madarasa kwenye shule yao.

    Reli ya kati ya Naivasha na mji mkuu Nairobi, inapita umbali wa kilomita moja hivi kutoka kwashule hiyo.

    Awali wanafunzi walisomea kwenye madarasa ya mabati na hali haikuwa salama hasa wakati wa joto au mvua.

    Lakini sasa mwalimu wao mkuu bwana Peter Kiwara anafurahia mazingira mapya na gredi za wanafunzi shuleni humo zimeongezeka.

    "Kampuni ya kujenga reli ya China ilitusaidia kujenga madarasa matatu yenye nafasi zuri ya kusomea wanafunzi . Sasa wanasoma vizuri na wamejikinga na jua kali au baridi wakati wa mvua. Idadi ya wanafunzi pia imeongezeka na wanafunzi wana hamu ya kusoma kwa bidii ili wawe wahadisi wa SGR siku za baadaye. Naweza kusema shule ya AIC Kitet imeimarika na SGR"

    Mama Sera Lenyapaa ni mzazi na ana watoto watatu kwenye shule ya msingi ya Kitet.

    "Nimeshukuru kampuni ya reli ya China kwa sababu wametujengea shule, watoto wanasoma vizuri"

    Ujenzi wa madasa kwenye shule hii ni sehemu ya mpango wa CRBC wa kuleta tabasamu kwa jamii zinazoishi karibu na reli.

    "Tunatenga asilimia 0.5 ya bajeti ya mradi wetu kwa shughuli za kusaidia jamii. Lakini pia itategemea na ukumbwa na mahitaji ya msaada tanaolenga kutoa kwa jamiii husika. Tunaweza kuongeza bajeti yetu, na miradi kwa jamii ."

    Kwenye awamu ya kwanza ya reli kutoka Mombasa hadi Nairobi zaidi ya wafanyakazi 1,000 wenyeji wamepokea mafunzo.

    Na kulingana na ripoti ya CRBC, kufikia mwishoni mwa mwaka 2017 zaidi ya wakenya 850 wamepokea mafunzo maalum yanayohuaiana na oparesheni za reli kama vile, ukarabati, umeme na mitambo.

    Bibi Sun Baohong ni balozi mpya wa China nchini Kenya.

    "SGR ni moja wa mifano inayong'aa kwamba kampuni za China nchini Kenya zinahusisha kazi za wajibu kwa jamii kwenye miradi yake. Kasi na ubora wa ujenzi wa reli ni za kuridhisha. Kwa jumla mradi huu wa reli umefungua zaidi ya nafasi 70,0000 za ajira na kutoka mafunzo kwa zaidi ya wakeya 5,000. Pia CRBC imetoa msaada wa masomo kwa wanafunzi zaidi ya 100 kupata elimu ya juu kuhusu maswala ya reli latika chuo kikuu cha Jiaotong"

    Ili kusaidia ukuaji wa viwanda vya ndani ya nchi na uchumi wa Kenya kampuni ya CRBC pia inanunua baadhi ya maligafi zake nchini humo.

    Mwaka 2017 ilinunua zaidi ya tani milioni moja za saruji na tani 90,000 za chuma nchini Kenya miongoni mwa bidhaa nyingine.

    Awamu ya 2A ya reli kati ya Nairobi na Naivasha inatarajiwakukamilikaJuni mwaka ujao.

    Inagharimu dola bilioni 1.4 na zaidi ya wakenya 46,000 wameajiriwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako