• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano kati ya China na Ulaya waweka mfano wa kukabiliana na mgogoro wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-06-26 08:18:49

    Mazungumzo ya saba ya ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Ulaya yamefanyika jana mjini Beijing.

    Mazungumzo hayo yakiwa ni utaratibu wa ngazi ya juu zaidi wa mawasiliano kati ya China na Ulaya juu ya masuala ya uchumi na biashara, yaliendeshwa kwa pamoja na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He na naibu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jyrki Katainen.

    Mazungumzo hayo yamepata mafanikio na kufikia makubaliano mengi, ambapo China na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuwa ni lazima zipinge kithabiti hatua za upande mmoja na za kujilinda kibiashara, na kuahidi kulinda kwa pamoja utaratibu wa biashara ya pande nyingi kwa kuliweka Shirika la biashara duniani WTO kama kiini, na kufuata msingi wa kanuni za shirika hilo, ili kukamilisha mfumo wa usimamizi wa mambo ya uchumi duniani. Makubaliano hayo yameonesha nia ya pamoja ya China na Umoja wa Ulaya ya kukabiliana na hatua za kibiashara za Marekani, na wazo la kuwajibika la pande hizo mbili, yakiwa makundi mawili muhimu ya uchumi duniani.

    China na Ulaya zikiwa ni wahimizaji na wanufaika wa utandawazi duniani, zote hazitaki vita ya biashara. Lakini kama Marekani itaendelea na hatua za upande mmoja, zitalazimika kuijibu na kujilinda. Muhimu zaidi ni kuwa, thamani ya jumla ya uchumi wa China na Umoja wa Ulaya inachukua asilimia 40 ya uchumi wa dunia, makubaliano hayo kati ya pande hizo mbili, si kama tu yameongeza imani ya dunia ya kupambana na hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara, bali pia yameleta utulivu kwa mfumo wa kimataifa unaokabiliwa na msukosuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako