• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali yapanga kushirikiana na sekta binafsi Uganda

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:34:29

    Wafanyabiashara nchini Uganda wanaitaka serikali kufadhili biashara ndogo na zile za wastani na pia kuzisaidia kupata mikopo ili kujiendeleza.

    Nayo serikali kupitia Shirika la maendeleo la Uganda, UDC limesema kwenye mpango wake wa kimkakati kwamba linahitaji angalau shilingi bilioni 500 kufadhili miradi ya muungano kati ya serikali na sekta binafsi.

    UDC imesema miradi inayolengwa ni kama vile kilimo-usindikaji na viwanda.

    Miongoni mwa maeneo mengine ambako serikali ingependa kuingia ubia na sekta binafsi ni pamoja na kufufua kiwanda cha saruji cha Moroto Ateker, kiwanda cha vioo cha Victoria Glass Works, kiwanda cha chumvi cha Katwe na kile cha matunda cha Soroti.

    Mwezi uliopita wakati mkutano wa 8 wa ushindani wa kitaifa waziri wa fedha Matia Kasaija alizindua Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako