• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki ya Dunia yaipa Kenya mkopo wa shilingi bilioni 20

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:35:15

    Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo wa Shilingi bilioni 20 kwa Kenya ili kusaidia kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na majanga.

    Fedha hizo zitatumika kutoa misaada kwa haraka wakati wa dharura za kiafya au majanga.

    Fedha hizo pia zitasaidia mageuzi muhimu ili kuimarisha uwezo wa Kenya wa kusimamia athari mbaya za kiuchumi na wale walioathirika.

    Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Kenya Diarietou Gaye amesema wanafanya kazi kwa karibu na wizara ya fedha ili kusaidia serikali kujikinga na hasara za kiuchumi zilizosababishwa na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.

    Kwa mujibu wa Uchunguzi wa Uchumi wa 2017, wakulima wa Kenya walipoteza zaidi ya Shilingi bilioni 16 mwaka 2016, kutokana na kupungua kwa mvua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako