• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam asifu juhudi zilizofanywa na mkoa wa Xinjiang katika kulinda haki za elimu kwa wanawake na watoto

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:44:41

    Kaimu mkuu wa kitivo cha Siasa na Utawala wa Jamii katika Chuo Kikuu cha Xinjiang Bi. Zuliyati Simayi amesema mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang umepiga hatua kubwa katika kulinda haki za wanawake na watoto kupata elimu.

    Bi. Zuliyati amesema hayo katika mjadala wa kawaida wa 38 wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Geneva. Amesema haki ya elimu kwa wanawake na watoto katika mkoa huo imehakikishwa, hivyo kuonyesha taswira ya mafanikio ya maendeleo ya haki za binadamu katika mkoa huo.

    Mtaalam huyo amesema China imeanzisha mfululizo wa sheria na kanuni kutokana na katiba ili kuhakikisha haki na matakwa ya wanawake na watoto wa makabila yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako