• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Taifa yajiandaa na mechi za kufuzu kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2018-06-27 09:37:41

  Timu ya taifa ya wanawake ya mchezo wa netiboli ya Uganda imeanza maandalizi kwa ajili ya mechi za kufuzu kombe la dunia mwaka 2019.

  Timu hiyo yenye wachezaji 19, imeanza mazoezi ya awali mjini Kampala kwa ajili ya mechi hizo za kufuzu zitakazofanyika nchini Zambia kuanzia Agosti 13 hadi 18.

  Kwa kuwa tayari timu sita zimekwishafuzu, tano ikiwa ni kutokana ubora wa viwango kwenye mchezo huo duniani, ikiwa ni pamoja na Uingereza ambao ni wenyeji wa mashindano, timu zingine kumi ndizo zitashindana ili kujaza nafasi zilizosalia.

  Uganda ambayo inashika nafasi ya saba katika viwango vya ubora duniani, nayo itashindana na baadhi ya timu kutoka kanda ya Afrika kwa ajili ya kufuzu mashindano hayo ambayo yataanza Julai 12 mwaka 2019 nchini Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako