Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuimarisha ushirikiano katika kupambana na magendo ya dawa za kulevya.
Tarehe 26 ilikuwa siku ya kupiga marufuku dawa za kulevya, ambapo Bw. Guterres ametoa hotuba akisema, suala la dawa za kulevya ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili binadamu, na linaathiri usalama na maendeleo endelevu.
Amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji ushirikiano wa kimataifa, na amezihimiza nchi zote zisitumie ovyo dawa, kueneza kilimo cha mimea mbadala ya mimea ya dawa za kulevya, na kuzuia magendo ya dawa za kulevya na uhalifu uliopangwa.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |