• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Watumishi wa umma kupunguziwa mishahara

    (GMT+08:00) 2018-06-27 19:40:29

    Watumishi wa umma nchini Kenya watapunguziwa mishahara kuanzia mwaka ujao kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya fedha.

    Pendekezo hili linajiri baada ya kugunduliwa kwamba watumishi wa umma wamekuwa wakikwepa kulipa fedha za baada ya kustaafu.

    Mishahara itakayokatwa itatumika kulipia pensheni zao pamoja na serikali kupunguza matumizi yao.

    Waalimu na maafisa wa usalama ni miongoni mwa watakapunguziwa mishahara.

    Kulingana na Kamau Thuge katibu mkuu wa wizara ya fedha ni kuwa awali mishahara hiyo ilitarajiwa kupungfuzwa kuanzia Septemba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako