• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Afrika Mashariki ya kuimarisha ushirikiano wa uchumi

    (GMT+08:00) 2018-06-27 19:41:21

    Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa mwito kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana kwa karibu zaidi ili kutumiza malengo yao.

    Akizungumza katika kongamano la 14 la miradi muhimu jijini Nairobi Kagame ameshinikiza kuwepo kwa utekelezaji wa miradi ya pamoja itakayoleta maendeleo ya maisha ya watu.

    Jumuiya ya EAC imekubaliana kuhusu biashara ya pamoja,uwekezaji na ushirikiano wa soko la pamoja.

    Aidha viongozi walizungumzia maendeleo ya miradi iliyoahidiwa katika kongamano la awamu ya 13 .

    Mada kuu ya kongamano la mwaka huu ni kuunganishwa kwa mradi wa reli ya kisasa inayotakiwa kuunganishwa kutoka Mombasa Kenya kupitia Kigali hadi Kampala.

    Kongamano hilo lilihudhuriwa pia na Rais Uhuru Kenyatta

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako