• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:EAC yazingatia sahali ya ushuru

    (GMT+08:00) 2018-06-27 19:56:56

    Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimepunguza baadhi ya kodi katika bajeti zao mwaka wa fedha 2018/2019.

    Unafuu wa kodi umeonekana katika bajeti zilizosomwa hivi karibuni na mawaziri wa fedha kutoka Tanzania, Kenya Uganda na Rwanda.

    Hayo yameonekana katika bajeti zilizosomwa hivi karibuni na mawaziri wa fedha kutoka nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Rwanda. Nchi hizo nne kati ya sita za EAC zina ajenda moja, ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuzalisha ajira za kutosha kwa wananchi hasa vijana ili kuwaondoa katika lindi la umasikini.

    Nchi nyingine wanachama EAC ambazo bajeti zake hazijasomwa ni Burundi na Sudan Kusini. Ili kutekeleza vipaumbele vya ukuaji wa uchumi wa viwanda kwa ufanisi, bajeti zote zimelenga katika kufyeka kabisa kodi ili kurahisisha uwekezaji katika sekta lengwa ya viwanda. Mathalani, Tanzania katika kuhimiza uchumi wa viwanda serikali imeondoa kodi kwa viwanda vya madawa hasa vifungashio vinavyotengenezwa kwa ajili ya sekta ya dawa.

    Wataalamu wa viwanda wanasema hatua hiyo ni ya kuhamasisha wawekezaji na wajasiriamali. Pia Serikali ya Tanzania imeondoa kodi katika manunuzi ya taulo za kike hali iliyosifiwa na kupongezwa na wanaharakati wa kijinsia wakisema itapunguza bei kwa bidhaa hizo na kuwafanya wananchi wote kumudu kununua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako