• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania yapongezwa katika usawa wa mapato kwa wananchi

    (GMT+08:00) 2018-06-27 19:57:21

    Tanzania imetajwa kupiga hatua kubwa katika kutekeleza matakwa ya Umoja wa Mataifa (UN) katika kustawisha usawa wa kipato kwa wananchi wake, ikilinganishwa na nchi zingine, hatua inayotokana na usimamizi mzuri katika mfumo wa maendeleo endelevu ya binadamu.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali.

    Mkutano huo ulizijumuisha taasisi za kifedha, utafiti, sekta binafsi, vyuo vikuu na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali ili kujadili maendeleo ya kiuchumi kulingana na Sera ya Kimataifa juu ya Masuala ya Maendeleo Endelevu (SDGs) Profesa Mkenda alisema kulingana na matakwa ya Umoja wa Mataifa kuhusu SDGs ambao Tanzania iliusaini, kwa kiasi kikubwa utekelezaji wake umeweza kufikiwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kupunguza tofauti ya kipato katika makundi yote sanjari na ukuzaji wa uchumi.

    Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema Tanzania ukiacha eneo la kiuchumi ambalo Tanzania imeonekana kufanya vizuri, pia inafanya vizuri katika kupunguza umasikini wa wananchi wake sambamba na kusimamia vyema suala la utunzaji wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako