• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wajasiriamali wa Afrika wapata mafunzo ya biashara kupitia Internet nchini China

  (GMT+08:00) 2018-06-27 20:53:12

  Wajasiriamali 29 kutoka Afrika wanashiriki mafunzo ya biashara kupitia mtandao wa Internet nchini China, ambayo yameandaliwa na kampuni ya Alibaba na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

  Naibu mwenyekiti wa kampuni ya Alibaba ambaye pia ni kiongozi wa mradi huo Bw. Huang Mingwei amesema, hali ya Afrika kwa sasa ni sawa na ilivyokuwa China miaka 10 iliyopita, hivyo uzoefu wa makampuni ya China huenda utatoa mafunzo kwa nchi za Afrika. Amesema China pia ingejifunza kutoka nchi za Afrika kwa kiwango cha juu cha matumizi ya Internet.

  Mafunzo hayo yanafanyika mjini Hangzhou kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 29 mwezi huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako