• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na waziri wa ulinzi wa Marekani

  (GMT+08:00) 2018-06-27 21:01:36

  Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis.

  Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Marekani ni moja ya uhusiano muhimu zaidi kati ya nchi mbili duniani, nchi hizo mbili zina maslahi makubwa ya pamoja katika sekta mbalimbali. Wakati huo huo si rahisi kuepuka kuzungumzia maoni tofauti kati ya nchi hizo mbili, na kusema China ina msimamo thabiti na dhahiri katika suala la mamlaka na ukamilifu wa ardhi. Aidha, rais Xi amesema uhusiano wa kijeshi ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Marekai, katika miaka ya hivi karibuni, na uhusiano huo umedumisha mwelekeo mzuri.

  Bw. Mattis amesema Marekani inatilia maanani uhusiano kati yake na China na uhusiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, na uhusiano wa kijeshi ni muhimu sana katika uhusiano kati ya pande hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako