• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri wa ulinzi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-28 10:21:24

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw James Mattis mjini Beijing.

    Rais Xi amesema maendeleo, mageuzi na marekebisho makubwa yametokea duniani hivi karibuni. Mwelekeo wa pande nyingi duniani na utandawazi umejikita, na nchi zote duniani zimekuwa zinajitegemea zaidi. Ameongeza kuwa China itaendelea kufuata njia ya maendeleo ya amani badala ya njia ya kujipanua na ukoloni, pia haitaleta vurugu duniani.

    Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Marekani ni moja ya mahusiano muhimu zaidi duniani, ambao unawanufaisha wananchi wa nchi zote mbili na watu wote duniani. Pia unasaidia kudumisha amani, utulivu na ustawi wa kimataifa na kikanda. Amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuhimiza maendeleo kwa kushikilia kanuni ya kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako