• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya biashara ya China yasema hatua ya Marekani ya kuzuia baadhi ya bidhaa kuuzwa kwa China itajidhuru

  (GMT+08:00) 2018-06-28 16:17:14

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, Marekani inatumai kuuza bidhaa nyingi zaidi kwa China, ili kupunguza urari mbaya wa biashara, lakini wakati huo huo inazuia baadhi ya bidhaa zake kuuzwa kwa China. Bw. Gao amesema kwa kufanya hivyo Marekani inajidhuru yenyewe.

  Hivi leo suala la biashara kati ya China na Marekani linafuatiliwa zaidi katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na wizara ya biashara ya China, msemaji wa wizara hiyo Bw. Gao Feng anasema,

  "tangu mwanzo kampuni za China na Marekani zimefanya ushirikiano kwa mujibu wa sheria, ushirikiano ambao umehimiza ongezeko la biashara na maendeleo ya teknolojia, na kunufaisha nchi hizo mbili. Marekani inatumai kuuza bidhaa nyingi zaidi kwa China, ili kupunguza urari mbaya, wakati huo huo inazuia baadhi ya bidhaa zake kuuzwa kwa China, na inajidhuru kwa kufanya hivyo."

  Takwimu zinaonesha kuwa katika miezi mitano iliyopita mwaka huu, uwekezaji wa China nchini Marekani ulikuwa dola za kimarekani bilioni 1.8, na kupungua kwa asilimia 92 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Bw. Gao anasema,

  "Tunafahamu kuwa baadhi ya mashirika ya kimataifa yakiwemo yale ya China yana wasiwasi kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini Marekani. Vitendo vya kujilinda kibiashara vya nchi hiyo vimeathiri uwekezaji wa kuvuka mpaka na ongezeko la uchumi wa dunia."

  Bw. Gao amesema, China siku zote inaona inapaswa kurahisisha uwekezaji wa kimataifa kwa mfululizo, na haikubali kuongeza masharti dhidi ya uwekezaji wa nchi za nje kwa kisingizio cha usalama wa taifa. Anasema,

  "Tumetambua kuwa katika mkutano wa kilele wa uwekezaji uliofanyika nchini Marekani, wajumbe wa baadhi ya majimbo wameeleza kukaribisha uwekezaji kutoka China, wakati huo huo, tuna wasiwasi kuhusu mabadiliko ya mara kwa mara ya sera ya uwekezaji wa Marekani. Wawekezaji wa kimataifa wataikimbia nchi hiyo kutokana na mabadiliko hayo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako