• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Afrika watumai China na Afrika kuimarisha ushirikiano ili kulinda usalama na utulivu wa kikanda

    (GMT+08:00) 2018-06-28 16:29:16

    Maofisa wa jeshi kutoka Afrika wanaohudhuria kongamano la ulinzi na usalama kati ya China na Afrika wamesema kongamano hilo linaonyesha maendeleo ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Afrika, na litahimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika amani na utulivu wa kikanda.

    Ofisa wa jeshi wa ubalozi wa Sudan nchini China Bw. Tilal Ali Alrayah Alsiddig amesema, ushirikiano wa ulinzi kati ya China na Afrika utanufaisha pande mbili.

    "Tunajua China siku zote inapendekeza ushirikiano wa kunufaishana, pia inaheshimu msimamo wa Afrika kuhusu ulinzi na usalama. China na Afrika zitanufaishana kutokana na matokeo yanayopatikana katika kongamano hilo, na ushirikiano wa ulinzi utahimiza maendeleo ya jumla ya majeshi ya nchi za Afrika, China pia itanufaika kwa uzoefu wa kijeshi wa nchi za Afrika. Lengo la hatua mbalimbali za kijeshi za China ni kulinda amani, ambalo linashikiliwa na China kwa siku zote. Kwa sasa umuhimu wa ulinzi wa jeshi la China umeonekana katika mambo ya kulinda amani barani Afrika."

    Wajumbe wanaohudhuria kongamano hilo wanajadili suala la usalama, ujenzi wa uwezo wa usalama barani Afrika, na ushirikiano wa ulinzi wa usalama kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako