• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waraka rasmi kuhusu China na WTO watolewa

    (GMT+08:00) 2018-06-28 17:36:40

    Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka rasmi uitwao "China na Shirika la Biashara Duniani".

    Waraka huo umesema, serikali ya China imechapisha waraka huo ili kutoa maelezo kamili ya China kutimiza ahadi zake kwa WTO, kufafanua kanuni, msimamo, sera, na mapendekezo ya China kuhusu mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kuelezea mtazamo na vitendo vya China katika kuendeleza mageuzi ya ngazi ya juu na ufunguaji mlango.

    Waraka huo umesema, China imetimiza ahadi zake kwa WTO, imefungua soko lake kwa dunia, na kuleta mafanikio ya pamoja kwa kiasi kikubwa. Kupitia juhudi hizo, China imetimiza wajibu wake kama nchi kubwa, na kwamba China inaunga mkono kithabiti mfumo wa biashara ya pande nyingi na imetoa mchango mkubwa kwa dunia baada ya kujiunga na WTO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako