• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Ushuru wa kampuni za kamari kuongezwa hadi asilimia 35

    (GMT+08:00) 2018-06-28 21:03:58

    Wabunge nchini Kenya wamekataa kata kata kupunguza ushuru wa kamari hadi asilimia 15 kutoka pendekezo la asilimia 35.

    Wiki hii wabunge hao kwa pamoja wamepiga kura ya kukataa kupunguzwa kwa ushuru wa kamari.

    Hii inamaanisha mashirika ya kamari sasa yatalazimika kulipa ushuru kwa serikali kwa kila mteja wao atakaeshiriki kucheza.

    Wamiliki wa kampuni hizo wamedai kwamba ushuru huo sasa utachangia kuzuka kwa kampuni feki za kamari zitakazokwepa kulipa.

    Kampuni hizo aidha zitatakiwa kuendelea kulipa asilimia 30 ya ushuru wa leseni na kushurutishwa kutumia asilimia 5 ya mapato yao kwa sghuhuli za michezo nchini.

    Sheria hiyo mpya itaanza kutumika Januari mwaka ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako