• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Uganda itapewa bilioni 7 za maendeleo ya uchumi

    (GMT+08:00) 2018-06-28 21:05:29
    Serikali ya Norway imeahidi kutoa shilingi bilioni 7.7 kwa afisi ya urataibu ya Umoja wa Mataifa nchini Uganda katika harakati za kuleta mabadiliko ya uchumi.

    Fedha hizo zitatumika kwa ushirikiano wa kufikia maendeleo ya millenia Uganda.

    Rosa Malango mratibu mkuu wa UN nchini Uganda anasema Uganda itatekeleza mabadiliko ya kiuchumi kupitia kwa miradi ya kuinua jamii na kuwaondoa kwenye umaskini.

    Mbali na hayo mashirika ya utumishi wa umma yameitaka serikali ya Uganda kuwasimamia kifedha wakimbizi kwa ajili ya kuwasaidia kuleta maendeleo nchini humo.

    Mwenyekiti wa mashirika hayo Julius Mukunda amesema wakimbizi wawekewe bajeti yao rasmi kuwapunguzia majanga ya kifedha na kuwawezesha kimaisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako