• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michuano ya Kombe la dunia 2018: Nidhamu imewaondoa Senegal

  (GMT+08:00) 2018-06-29 09:27:45

  Alhamisi ya Jana bara la Afrika lilikuwa na imani kuwa timu ya taifa ya Senegal ndio litakuwa taifa pekee la Afrika kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia 2018, hiyo ni baada ya kuingia uwanjani kupambana dhidi ya Colombia ikiwa inahitaji point moja.

  Colombia kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Yerry Mina dakika ya 74, limewafanya Senegal kuaga michuano hiyo licha ya kufanana kila kitu na Japan waliofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora.

  Japan anafuzu kwa kipengele cha fair play ikiwa na maana kuwa Japan wameoneshwa kadi chache za njano zaidi ya Senegal waliofanana nao kila kitu, hivyo sasa ni wazi timu zote 5 zilizokuwa zinaiwakilisha Afrika zimetolewa katika hatua ya makundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako