• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la maendeleo ya kidijitali ya televisheni la Afrika lahimiza ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-06-29 10:29:05

    Kongamano la nane la maendeleo ya kidijitali ya televisheni la Afrika limefanyika hapa Beijing, ambapo wajumbe kutoka nchi 43 za Afrika, nchi 5 za Asia na China wamejadili mpango wa maendeleo ya kidijitali katika radio na televisheni barani Afrika, na kuhimiza ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na nchi za Afrika.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongomano hilo, naibu mkurugenzi wa ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China Guo Weimin amesema vyombo vya habari ni njia muhimu ya kuzidisha urafiki kati ya watu wa China na Afrika, na pia ni daraja muhimu la kuhimiza mawasiliano ya kibinadamu kati ya pande hizo mbili, na inatarajiwa kuwa kongamano hilo litahimiza maendeleo ya kasi ya kidijitali ya televisheni barani Afrika na kufanya teknolojia ya habari na mawasiliano ya kisasa yawanufaishe Waafrika.

    Mkurugenzi wa kampuni ya Startimes ya China Bw. Pang Xinxing amesema kampuni yake inapenda kuwa daraja na balozi wa mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika, na kuzisaidia nchi za Afrika zipate maendeleo ya kidijitali kwenye radio na televisheni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako