• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza orodha hasi mpya kwa uwekezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2018-06-29 10:40:59

    China imetangaza orodha hasi iliyorekebishwa kuhusu uwekezaji kutoka nje, ambayo maeneo yanayozuiwa kwa wawekezaji wa kigeni yamepunguzwa kutoka 63 hadi 48 ya sasa.

    Orodha hiyo iliyotolewa kwa pamoja na Kamati ya taifa ya maendeleo na mageuzi na Wizara ya biashara, itaanza kutekelezwa Julai 28.

    Orodha hiyo mpya imepanua upatikanaji wa soko kwa uwekezaji kutoka nje nchini China, ikiwa na hatua 22 za kufungua mlango kwenye sekta za uchukuzi, huduma za kitaaluma, miundombinu, nishati, raslimali na kilimo.

    Kwa mujibu wa kamati ya mageuzi na maendeleo ya China, orodha hiyo pia imeweka ratiba ya kufungua sekta za magari na fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako