• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vipepeo wanaweza kuvuka jangwa la Sahara

    (GMT+08:00) 2018-06-29 14:15:52

    Je unajua vipepeo wanaweza kusafiri kwa umbali gani? Utafiti unaonesha kuwa vipepeo aina ya Painted lady wanahama kati ya Ulaya na Afrika na kuvuka jangwa la Sahara mara mbili kila mwaka.

    Vipepeo hao wanaonekana kwa wingi duniani, urefu wa mabawa yao ni sentimita 5 hadi 7, mabawa yake ni mekundu, yana madoa meusi, ncha za mabawa ni nyeusi, na zina madoa meupe.

    Utafiti uliofanyika zamani unaonesha kuwa vipepeo hao wanaoishi kusini mwa Ulaya wanahamia sehemu ya kati ya Afrika katika majira ya mpukutiko, lakini watafiti hawakujua baadaye vipepeo hao na watoto wao wanakwenda wapi.

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani na wenzao wa nchi mbalimbali wamechunguza vipepeo wanaoishi karibu na bahari ya Mediterranean katika majira ya mchipuko kwa miaka kadhaa mfululizo, wamekusanya sampuli za kikemikali kwenye mabawa ya vipepeo, kutafiti idadi ya vipepeo, upande wa wanaoruka na upepo, na kuthibitisha kuwa karibu nusu ya vipepeo walitoka kusini mwa jangwa la Sahara.

    Umbali wa safari ya vipepeo unaweza kufikia kilomita elfu 12. Safari ya kwenda na kurudi humalizwa na vipepeo wa vizazi kadhaa, lakini vipepo wachache wanaweza kumaliza safari hii pekee yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako