• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China kufanya ziara barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-06-29 16:59:27

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atafanya ziara rasmi nchini Bulgaria na Ujerumani kuanzia tarehe 5 hadi 10 mwezi ujao, ikiwa ni shughuli muhimu ya kidiplomasia ya China barani Ulaya tangu serikali mpya ya China iingie madarakani mwezi Machi mwaka huu.

    Akiwa nchini Bulgaria, Bw. Li atakutana na rais Rumen Radev wa nchi hiyo na waziri mkuu Bw. Boyko Borisov, ambapo viongozi hao watabadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, na namna ya kuongeza ushirikiano kutokana na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na utaratibu wa Nchi 10 +1. Bw. Li pia atahudhuria mkutano wa 7 wa viongozi wa China na nchi za Ulaya ya Mashariki.

    Nchini Ujerumani, Bw. Li atakutana na rais Frank-Walter Steinmeier na kufanya mazungumzo na chansela wa nchi hiyo Bibi Angela Merkel, na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano mbalimbali ya ushirikiano wa kibiashara. Aidha, Bw. Li na Bibi Merkel wataendesha kwa pamoja mazungumzo kati ya serikali za China na Ujerumani ambayo yatahudhuriwa na mawaziri zaidi ya 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako