• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyama tawala vya nchi za Afrika mashariki vyakipongeza chama cha CPC cha China kwa mwongozo wake wa kuhudumia umma

  (GMT+08:00) 2018-06-29 17:26:05

  Viongozi wa vyama tawala vya nchi nne za Afrika Mashariki Tanzania, Kenya, Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC wamekipongeza chama cha kikomunisti cha China CPC kwa miongozo yake ya kuzingatia maslahi ya umma, na mafanikio kiliyopata tangu kilipoanzishwa miaka 97 iliyopita, na kusema vyama vyao vinapaswa kuiga uzoefu wa chama cha CPC.

   

  Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi cha Tanzania CCM Bw. Bashiru Ally alipohojiwa na mwanahabari wetu amesema, CCM na chama cha CPC cha China vina misimamo inayofanana kuhusu njia ya kuendeleza nchi, na vyama vyote viwili vinaamini kuwa maendeleo yoyote yanatakiwa kuhudumia maslahi ya umma, na hii ndio ni njia pekee ya kuuondoa umma kutoka kwenye umaskini, ujinga na maradhi, na hatimaye kuelekea maisha bora.

  "Kwa kipindi cha miaka 97 ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China, China imepiga hatua kubwa sana, na idadi kubwa ya wachina imeondoka kutoka lindi la umaskini. Msingi mkubwa wa maendeleo ya China ni kwa wachina wenyewe kujiamini, wanatengeneza mitindo na taratibu na mikakati ya maendeleo, kwa kulingana na hali yao halisi. Wanajenga ujamaa kwa mujibu wa historia na mahitaji yao. Kwa hiyo siku zote wamekuwa na uongozi safi, siasa safi na serikali safi."

  Katibu mkuu wa muungano tawala wa Jubilee wa Kenya Bw. Raphael Tuju amesema, chini ya uongozi madhubuti wa nadharia na fikra zake, chama cha kikomunisti cha China kimeongoza watu wa China kupata mafanikio makubwa katika kujenga na kuendeleza nchi, na chama tawala cha Kenya kinapaswa kujifunza uzoefu wa CPC, ili kuisaidia Kenya itimize lengo lake la kuwa nchi ya viwanda.

  Sauti 2

  "Tuna mengi ya kujifunza ili katika kizazi kimoja tunaweza kufikia mabadiliko kama hayo. Kwanza kabisa ni kuhusu jinsi wanavyoweka chama chao kuwa pamoja na wananchi, ili chama kiweze kujengwa kwenye msingi imara wa kiitikadi."

  Naibu katibu mkuu wa chama cha Harakati ya Upinzani ya kitaifa cha Uganda (The National Resistance Movement Organization, NRM) Bw. Richard Todwong amesema, katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleze sera ya mageuzi na kufungua mlango, haswa baada ya kufanyika kwa Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, chama cha CPC kimethibitisha wazi uhodari wake katika kuongoza na kutawala nchi, na chama cha NRM kinakubali kabisa mtizamo wa chama cha CPC kuhusu utawala wa nchi, na kinatarajia kuimarisha ushirikiano na mawasiliano na chama cha CPC kwenye nyanja za kupunguza umaskini na kuleta maendeleo endelevu.

  Sauti 3

  "China ilipambana na umaskini kwa sababu maeneo ambayo waliyazingatia zaidi yalikuwa maeneo ambayo yaliiathiri jamii. Wameonyesha kwamba, ni watu halisi na muafaka ambao tunaweza kushughulika nao, wakiwa watu ambao wameondokana na umaskini, watu ambao wanafanya jitihada kubwa kuziletea maendeleo nchi zetu, wanatambua mambo yanayokwamisha maendeleo. Viongozi wao wamejiandaa, wanatambua hali za watu wao."

  Naibu katibu mkuu wa chama cha PPRD cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Bw. Ferdinand Kalumbi amesema, kikiwa ni muungano tawala wa DRC, PPRD kinalenga kujifunza uzoefu wa chama cha CPC cha China, kuhusu jinsi kilivyokabiliana na changamoto mbalimbali na kupata mafanikio makubwa ya maendeleo, na pia kinapaswa kujifunza kutoka kwa chama cha CPC kuhusu namna ya kuendeleza demokrasia ya umma na kupata uungaji mkono mkubwa wa umma.

  Sauti 4

  "Chama chetu cha PPRD pia tunapaswa kutekeleza mtizamo wa demokrasia kama ya chama cha Kikomunisti cha China, ambapo hata watu wa mashinani wanaweza kujua mikakati ya chama na maamuzi ya serikali, ili wote washikamane kwa pamoja katika kujenga uchumi, kuondoa umaskini, kuimarisha usalama na kunufaisha wananchi wote."

  Chama tawala cha Burundi CNDD/FDD na chama cha kikomunisti cha China CPC vimekuwa na uhusiano mzuri tangu zamani, na vimedumisha mawasiliano kupitia njia mbalimbali. Katibu mwenezi wa chama hicho Bibi Nancy Mutoni amesema, chama tawala cha Burundi kimejifunza uzoefu mwingi muhimu kutoka kwa chama cha CPC cha China, haswa mikakati yake ya kuendeleza na kusimamia sekta ya kilimo.

  Sauti 5

  "Tukiwa ni chama tawala cha Burundi, tumekuwa na ushirikiano wa karibu na chama cha CPC cha China. Kila mwaka vyama hii viwili vinatembeleana na kubadilishana maoni kuhusu utawala wa nchi, mapambano dhidi ya ufisadi na maendeleo ya vijijini. Mtindo wa maendeleo ya China umeweka mfano wa kuigwa kwa Burundi, na huu ni mtindo wa pekee unaoweza kustawisha uchumi wa Burundi. Tunapongeza sana ushirikiano kati yetu na China, kwa kuwa unalenga kutafuta maslahi ya umma."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako