• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakurugenzi watakiwa kutafuta wawekezaji

    (GMT+08:00) 2018-06-29 18:49:47

    Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Alexander Mnyeti amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Hanang, Mbulu, Kiteto, Babati na Simanjiro mkoani humo kutengeneza mazingira salama ya uwekezaji na kuweka mikakati ya kuwashawishi wawekezaji wawekeze katika maeneo yao.

    Alitoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa maendeleo mkoani humo cha kupokea taarifa ya tafiti ya fursa za uwekezaji kutoka TIRDO.Amesema Manyara iko nyuma kimaendeleo kutokana na viongozi kusubiri wawekezaji waje bila kuwashawishi na kuwawekea mazingira salama ya uwekezaji ya utoaji wa leseni na hati. Mnyeti amesema, serikali iko tayari kushirikiana na wawekezaji watakaofuata taratibu na sheria kwa kusikiliza wanasema nini kuhusu utoaji wa leseni na hati kupitia wakurugenzi watendaji wa halmashauri kuondoa urasimu usio wa lazima.Aidha mkuu huyo pia amekiruhusu kiwanda cha Malt Superbrand Limited mkoani humo kuendelea na uzalishaji wa bidhaa za vinywaji baada ya kufungwa na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa madai ya kuwa hawana kibali cha kutumia kemikali ambazo zinatumiwa katika utengenezaji wa bidhaa zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako