• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya hupoteza bilioni 200 kila mwaka kutokana na bidhaa gushi

    (GMT+08:00) 2018-06-29 18:50:44

    Serikali ya Kenya hupoteza Shilingi bilioni 200 kila mwaka kutokana na uingizaji wa bidhaa ghushi nchini.

    Hii ni licha ya mikakati ambayo imekuwepo katika juhudi za kukabiliana na bidhaa hizo.

    Hata hivyo, Mamlaka ya Kitaifa Kuhusu Bidhaa Ghushi Kenya (ACA) imesema kwamba imefaulu kunasa bidhaa za Sh1.8 bilioni, tangu operesheni dhidi yake kuanza mwaka huu.

    Kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuhusu Bidhaa Ghushi jijini Nairobi, mamlaka hiyo imesema kwamba imefaulu kuwakamata watu 1,200 kuhusiana na bidhaa hizo tangu mwaka 2011.

    Akihutubu kwenye maadhimisho hayo, Afisa Mkuu Mtendaji wa mamlaka hiyo, Elema Halake, amesema kuwa serikali imeimarisha juhudi zake za kukabili bidhaa hizo, kwani zinapunguza pato la jumla la kitaifa.Hayo yanajiri huku serikali ikiimarisha operesheni dhidi ya bidhaa hizo, chini ya uongozi wa jopo maalum lililobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta, chini ya uongozi wa Naibu Mkuu wa Utumishi wa Umma Wanyama Musiambo.

    Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ameapa kuendeleza operesheni hiyo hadi pale bidhaa hizo zitaisha nchini

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako