• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanuni ya kuwepo kwa China moja haijadiliki

    (GMT+08:00) 2018-06-29 19:22:39

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, kanuni ya kuwepo kwa China moja ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani, na haijadiliki.

    Bw. Lu Kang amesema kuwa, kuna China moja tu, na Taiwan ni sehemu moja ya China, hii ni hali halisi na inakubaliwa na jumuiya ya kimataifa. Idara ya safari za ndege za abiria ya China inayataka mashirika ya ndege ya Marekani kutumia "Taiwan China" badala ya "Taiwan", kwani hiyo itaonyesha msimamo thabiti wa serikali ya China katika kanuni ya kuwepo kwa China moja.

    Bw. Lu Kang amesema, China inakaribisha makampuni ya nchi za nje kuwekeza nchini China, lakini makampuni hayo yanapaswa kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, kufuata sheria ya China, na kuheshimu uzalendo wa watu wa China.

    Ubalozi wa Marekani nchini China jana imetoa taarifa ikisema China imekataa kujadiliana na Marekani kuhusu China kutaka mashirika ya ndege ya abiaria ya Marekani kutumia "Taiwan China" badala ya "Taiwan"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako