• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liang Jia He 1

    (GMT+08:00) 2018-07-01 19:02:00





    Tarehe 13 Februari,2015, yaani siku ya Tarehe 25 ya mwezi wa 12 kwa kalenda ya kilimo ya China, saa 5 asubuhi, Rais Xi Jinping alirudi Liang Jia He—kijiji kidogo kilichoko kwenye Uwanda wa Juu wa Udongo wa Manjano.
    "Jinping umerudi!"
    Wanakijiji wengi waliposikia sauti ya kuwashangaza walitoka nyumbani kwa kumkaribisha.
    Akifika kijiji hiki na kukutana na wanakijiji wengi Bw. Xi Jinping alisisimka sana, aliwahi kufanya kazi na kuishi kwenye kijiji hicho kwa miaka saba, na siku zote anakumbuka hali ya kijiji na hawezi kuwasahau wanakijiji wa huko.
    Mara wanakijiji walimzunguka Xi Jinping huku wakiongea naye. Walipofika mlango wa ofisi ya Kamati ya Kijiji, Xi Jinping akazungukwa na watu wengi zaidi, ambao walifurahi sana pia.
    Katibu mkongwa wa tawi la Chama la kijiji hiki Mzee Liang Yuming alichelewa kufika akajipenyeza mbele kwa nguvu, Xi Jinping alimsalimu na kupeana mkono naye kwa uchangamfu. Mzee Liang alimwambia: "Sasa narudi kwangu kuandaa chakula, baadaye tule pamoja."
    Xi Jinping alipiga soga na "wenzake wa utotoni" akiwauliza: Mapato yenu yanategemea kazi gani ? Siku za kawaida mnakula nini? Wazazi wenu hawajambo? Watoto wenu sasa wanafanya nini? Maisha yenu sasa ni ya hali gani? Sasa mnaweza kupata wali na nyama za kutosha? …
    "Wenzake wa utotoni" walimwambia: "Sasa tunaishi maisha mazuri, tunaweza kupata vyakula vya aina mbalimbali, tukipenda kila mara tunaweza kula wali na nyama."
    Xi Jinping aliposikia alitabasamu na kusema kwa maridhiko: "Vizuri, wanakijiji mnaweza kuishi maisha mazuri, mimi nafurahi sana."
    Xi Jinping aliondoka Liang Jiahe mwaka 1975. Hii ni safari yake ya pili ya kurudi kijijini humo. Wanakijiji walikumbuka kuwa, safari yake ya kwanza ya kurudi kijijini ni mwaka 1993.
    Tarehe 27 Septemba mwaka 1993, Xi Jinping alipokuwa Katibu wa kudumu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Fujiang,ambaye pia alikuwa katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Fuzhou, alirudi Kijiji cha Liang Jia He kwa mara ya kwanza. Alipofika kijijini alitembelea familia moja baada ya nyingine za wanakijiji, ambapo aliwawataka watu wote wakumbuke: "Si kama tu mnatakiwa kutatua kwanza tatizo la njaa, bali pia mnatakiwa kutilia maanani elimu." Alizawadia kila familia saa moja ya elektroniki ili watoto wao watumie kwa ajili ya kwenda shuleni, anatumai watoto waweze kupata elimu zaidi.
    Safari hii ya mwaka 2015 alirudi tena kijijini kabla ya Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa China, alitoa pesa zake mwenyewe akawanunulia wanakijiji michele, unga wa ngano, mafuta ya kupikia, nyama na vingine vingi, kila familia imepata zawadi.
    Xi Jingping alitembelea kijijini humo, kila eneo, na kuona mabadiliko mapya ya huko. Alipokuwa katibu wa tawi la Chama la Kikosi cha uzalishaji cha Liang Jia He aliwahi kuwaongoza wanakijiji kujenga upya mashamba yenye rutuba, ambayo yanaendelea kupandwa mimea ya chakula; na aliwahi kuwaongoza wanakijiji kujenga Dimbwi la gesi za vinyesi ili kupata nishati kwa ajili ya maisha ya wanakijiji, mpaka sasa bado yanawanufaisha wanakijiji.
    Machoni mwa wanakijiji, Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama Xi Jinping bado ni "Kijana huyu huyu aliyeweza kuvumilia taabu, kufanya kazi halisi na kupenda kusoma vitabu".
    Mwaka 1969 Xi Jinping alifika Liang Jia He kufanya kazi kijijini, baada ya miezi michache tu, akawa na mawasiliano ya karibu na wanakijiji, na kila mara aliwasaidia wanakijiji wenye taabu maishani. Na alipokuwa katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Fuzhou alimpokea mwanakijiji wa Liang Jia He aliyepata ugonjwa kutibiwa mjini humo, na kutoa pesa zake mwenyewe kumsaidia sana. Xi Jinping pia alisaidia kijiji hiki kupata umeme, kujenga shule na daraja, wanakijiji wote wanakumbuka sana msaada wake, walisema: Moyo wa Jinping uko Liang Jia He siku zote." Xi Jinping aliwahi kusema: "Wakati ule nilipofika kijijini nilikuwa na umri wa miaka 15, nilikuwa sijui kufanya kazi yoyote, wanakijiji walinifundisha kuishi maisha, kulima mashamba, hata kila mara waliniletea vyakula walivyopika. Niliishi pamoja na wanakijiji na kuzoea maisha ya huko, baada ya kuondoka huko bado siwezi kusahau kila kitu cha kijijini. Hivi sasa kila nilipoona raia wa sehemu zenye hali ya umaskini, kweli niliwahurumia sana, sisi wakomunisti, ni lazima tuwafuatilie zaidi raia hao, na kuwasaidia kutatua taabu, ama sivyo wema wetu utakuwa wapi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako