• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liang Jia He 2

    (GMT+08:00) 2018-07-01 19:23:18

    Tarehe 22 Desemba, mwaka 1968, mwenyekiti Mao Zedong alitoa wito: Vijana wasomi kwenda vijijini kuelimishwa tena na wakulima ni jambo la lazima". Wito huu ulipotolewa, mara wanafunzi vijana wa nchi nzima wapatao milioni 17 waliitikia na kuondoka mijini na kwenda vijijini kuanza kipindi kigumu cha maisha yao ambacho hawatakisahau.

    Kijana Xi Jinping alikuwa mmoja wa vijana hao, aliondoka mji mkuu Beijing akaenda Yanan, sehemu takatifu ya mapinduzi.

    Tarehe 13 Januari,1969, Xi Jinping aliyekuwa na umri chini ya miaka 16 alipanda garimoshi maalumu la "vijana wasomi" akaenda Yan'an.

    Siku chache baadaye "vijana wasomi" waligawanywa katika vikundi tofauti na kila kikundi kilipelekwa kwenye kijiji kimoja. Xi Jinping na vijana wengine 15 walipelekwa kwenye Kijiji cha Liang Jia He, na Xi Jinping alikuwa umri mdogo zaidi kuliko wengine. Katibu wa tawi la Chama wa wakati huo Mzee Liang Yuming anakumbuka kuwa, Xi Jinping alifika kijijini kwao na masanduku mawili, wanakijiji walimsaidia kubeba, na waliona ni mazito sana, walidhani ndani kuna vitu vyenye thamani, lakini baadaye waliona yamejaa vitabu.

    Wanakijiji wa Kijiji cha Liang Jiahe wanakumbuka kuwa, Xi Jinping alipofika huko aliwaachia picha ya kijana mrefu, mwembamba na mwenye ngozi nyeupe kiasi.

    Baada ya kufika Kijijini Liang Jia He, Xi Jinping alikuwa kama amebadilika kuwa kijana mwingine, alijitahidi kuondoa tofauti kati ya mzaliwa wa Beijing na mtoto wa kijijini, hayo ni mabadiliko magumu makubwa.

    Kwa Xi Jining, wakati alipokuwa kijijini Liang Jia He, kitu kilichomsumbua zaidi ambacho alikuwa hawezi kuvumilia kabisa ni wadudu viroboto. Xi Jinping ana aleji ya mdugu kiroboto, akiumwa ngozi yake mara ikavimba, akikwaruza aliona ngozi iliwasha sana, aliona uchungu sana. Bw. Shii Chunyang aliwahi kufanya kazi kijijini pamoja na Xi Jinping, aliona ngozi ya miguuni mwake ilibaki makovu mengi kutokana na kuumwa na viroboto.

    Kwa kuwa Xi Jinping aliyeishi kijijini hana "harufu ya mijini" akaelewana zaidi na vijana wa kijijini, kila mara aliwasaidia wenzake wenye taabu, baadhi ya wakati aliwasaidia kukata nywele, ama kuwafundisha kuogelea, vijana wengi kijijini wakawa marafiki zake. Na mawasiliano kati yao na Xi Jinping yaliwasaidia kuchagua vizuri maisha yao, rafiki yake Wu Hui baadaye akawa mwalimu, na Shi Chunhui alikuwa katibu wa tawi la Chama la Liang Jia He baadala ya Xi Jinping baada ya Xi kuondoka kijiji hiki.
    Wanakijiji walimsifu kijana huyu kutoka Beijing, na Xi Jinping alikuwa kama dirisha moja na macho mawili kwa wanakijiji kufahamishwa hali ya dunia nje ya kijiji chao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako