• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa ufunguzi wa mkutano wa kilele wa 31 wa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-01 19:55:58

    Rais Xi Jinping wa China leo ametuma barua ya pongezi kwa ufunguzi wa mkutano wa 31 wa kilele wa Umoja wa Afrika.

    Katika barua yake hiyo, Rais Xi Jinping amesema , Umoja wa Afrika unajitahidi kuhimiza mchakato wa utandawazi wa Afrika, nchi za Afrika zitaendelea kutoa sauti ya pamoja katika masuala makuu ya kimataifa na kikanda, uwezo wao wa kulinda amani na usalama umeongezeka zaidi. Amesema anatumai kuwa, Umoja wa Afrika utaongoza nchi za Afrika kupata mafanikio makubwa zaidi.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utafanyika mwezi Septemba mwaka huu, China itashirikiana na Afrika kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano na kimkakati kati ya China na Afrika kuinuka na kufikia kiwango kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako